Jumanne, Julai 29, 2014

WALEMAVU IRINGA KUFANYA SENSA NA MPANGO MADHUBUTI WA KUJISIMAMIA KUANZA

Chama cha watu wenye ulemavu wa kuona Mkoani Iringa kinatarajia kufanya sensa ya watu na makazi kwa ajili ya kuunda  vikundi vitakavyowasaidia kupata misaada toka katika mashirika mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa‭  ‬chama‭ ‬cha watu wenye ulemavu wa kuona (TLP) wilaya ya Iringa‭ ‬Mwl.‭ ‬Felix Mkini amesema sensa hiyo itaunda vikundi saba na baadhi ya vijiji ili  viweze kupata misaada itakayowasaidia kuanzisha shughuli za kijasiriamali ili waondokane na utegemezi.
Mwl.‭ ‬Mkini amesema sensa hiyo inatarajiwa kuanza Agosti‭ ‬20‭ ‬mwaka huu ambapo itakuwa chini ya Makatibu Kata na Tarafa wakishirikiana na wenyeviti wa‭  ‬serikali za mitaa ili kuweza kupata idadi yao kamili.
Aidha amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoshirikishwa katika miradi ya maendeleo kutokana na ulemavu walonao hali ambayo imepelekea kupata shida katika matumizi ya barabara.
Mwenyekiti wa chama hicho ameomba serikali kuvisaidia vikundi hivyo ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi hali ambayo itasaidia kuinua vipato vyao na kuondokana na utegemezi kwa jamii.
Hata hivyo.‭ ‬Mwenyekiti wa walemavu halmashauri ya wilaya ya Iringa Mwl.‭ ‬Felix Mkini ametoa wito kwa wakazi wa manispaa ya Iringa kuwapa ushirikiano watu wenye ulemavu kwa kuwapatia elimu.

0 comments:

Chapisha Maoni