Jumanne, Julai 29, 2014

ELIMU DUNI CHANZO CHA MAAMBUKIZI MAPYA YA HIV/AIDS

Uelewa mdogo wa elimu ya maambukizi na athari za ugonjwa wa Ukimwi umepelekea idadi kubwa ya vijana Mkoani Iringa kuendelea kuathirika na ugonjwa huu hali inayopelekea kupotea kwa nguvu kazi ya taifa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini Dkt Letisia Warioba amesema vijana wataondokana na tatizo hili kama watajilinda,kujipenda ikiwa ni pamoja na kushiriki upimaji wa hiari ambapo itawasaidia kujua hali zao na kuepuka maambukizi mapya ya Ugonjwa wa Ukimwi.
Dkt.Warioba ameongeza kuwa licha ya kushiriki shughuli za upimaji wa hiari baadhi ya vijana hao wamekuwa wakiondoka pasipo kusubiri ili waweze kupata majibu na ushauri nasaha kwenye vituo vya kutolea huduma hizo.
Naye Mratibu wa Tume ya kuthibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Bw .Saimon Kilario amesema elimu kuhusu maambukizi na athari za ukimwi zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kampeni ya SHUGA RADIO yenye lengo la kuongeza uelewa wa Ugonjwa wa Ukimwi.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini amesema Mkoa wa Iringa bila Ukimwi inawezekana hivyo ushirikiano wa kutosha kwa jamii na asasi zote za kiserikali na zisizo za kiserikali itapunguza ongezeko la ugojwa wa Ukimwi kwa Mikoa ya Nyanda za juu kusini ikiwepo mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya.

0 comments:

Chapisha Maoni