Liverpool watafanya jitihada za mwisho kujaribu kumshawishi Ashley Cole
kujiunga nao (Mail on Sunday), taarifa nyingine zinasema Cole tayari
ameingia mkataba wa miaka mitatu na Roma ya Italy (Sunday People),
Everton watatupilia mbali maombi ya Manchester City ya kumtaka Ross
Barkley (Liverpool Echo), boss wa Liverpool Brendan Rodgers atamruhusu
Martin Skirtel kuondoka iwapo atapata mtu wa kuziba nafasi yake, huku
Dejan Lovren wa Southampton akitazamwa
kuchukua nafasi hiyo (Sunday Express), beki wa Newcastle Matheiu Debuchy
amethibitisha kuwa atajiunga na Arsenal msimu ujao (Sunday Express),
Newcastle wanatazama uwezekano wa kumchukua beki wa kulia wa Ajax
Ricardo van Rhijn kuziba nafasi ya Debuchy (Metro), Liverpool watapewa
pauni milioni 75.5 na Barcelona za kumnunua Luis Suarez (Sunday Mirror),
kiungo wa zamani wa Chelsea Frank Lampard anakaribia kutangaza kujiunga
na New York City FC (Daily Star Sunday), meneja wa Arsenal, Arsene
Wenger anataka kumnunua, ama kiungo wa Real Madrid Sami Khedira au
Morgan Schneiderlin wa Southampton (Sunday Mirror), Juventus wanataka
kulipwa pauni milioni 45 pamoja na Luis Nani ikiwa Manchester United
wanamtaka kiungo Arturo Vidal (Daily Star Sunday), Barcelona wamekataa
kumsaini beki wa kati wa Liverpool, Daniel Agger, badala yake Barca
wanamtaka Mats Hummels (Mundo Deportivo), Juventus wanahaha kumsajili
Alexis Sanches lakini watalazimika kuuza wachezaji ili kupata fedha.
Juve watakuwa tayaru kuwauza Paul Pogba na Arturo Vidal (Tuttosport),
Liverpool huenda wakatumia sehemu ya pauni milioni 70 za Suarez,
kumnunua mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli, ambaye anataka sasa
kurejea EPL (Tuttosport), Newcastle United wanataka kumsajili winga wa
Manchester United Wilfried Zaha kwa pauni milioni 7. Zaha alinunuliwa na
Man U kwa pauni milioni 15 (Daily Mirror), Manchester United wamekataa
ombi la Southampton la kumsajili Javier Hernandez Chicharito (Sunday
People). Share tetesi hizi wa wapenda soka.




0 comments:
Chapisha Maoni