Liverpool inafikiria kumsajili mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli,
iwapo Luis Suarez atajiunga na Barcelona (Daily Express), Wakati huohuo
Brendan Rodgers anamtaka beki Dejan Lovren kuwa mchezaji wa tatu kutoka
Southampton kwenda Anfield, baada ya kumchukua Lambert na Lallana
(Times), kiungo wa Colombia James Rodrigues anajiandaa kuondoka Monaco
kwenda Real Madrid kwa pauni milioni 40, iwapo Real watamuuza Angel Di
Maria (Daily Mail), Arsenal watathibitisha
kumsajili Mathew Debuchy kutoka Newcastle baada ya Kombe la Dunia
(Daily Star), mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez amekiri kuwa
angependa kujiunga na Arsenal, klabu ambayo alikuwa akiishabikia akiwa
mtoto (Daily Express), Manchester City wamekubaliana na Roma kumsajili
beki wa kati Mehdi Benatia, lakini watasubiri Roma wapate mtu wa kuziba
pengo (Daily Mirror), kipa wa Costa Rica Keylor Navas anajiandaa kuhamia
England baada ya Arsenal nao kujiunga na Liverpool kumsaka (Daily
Star), Manchester United watatoa pauni milioni 20 kumsaka beki wa
Borussia Dortmund Mats Hummels wiki hii (Metro). Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni