Jumatano, Julai 02, 2014

SASA HII NDIO SINEMA NZIMA NA SAUTI ZA UGOMVI WA B12, MCHOMVU NA DJ FETTY KATIKA XXL YA CLOUDS FM LEO MCHANA

Katika shughuli zote za studio ya ' On Air' hakuna kitu cha muhimu na kinachopaswa kuangaliwa kwa umakini kama 'MICROPHONE' kwasababu si kila kitu kinachoongelewa studio kiende hewani na kusikilizwa na wasikilizaji, nasema hivyo kwasababu kosa la kuacha 'mic' hewani ni kitu kinachoweza kukusababishia matatizo makubwa!!!
Leo kama ulibahatika kusikiliza XXL ya Clouds fm basi utakuwa shahidi wa kilichotokea baada ya kufanyika kosa moja dogo la kuacha mic 'on' na kuendelea na ubishani uliopelekea ugomvi mkubwa ndani ya studio hizo za Clouds Fm, na ugomvi wenyewe ulikuwa ni kati ya watangazaji wa kipindi hicho B12, Adam Mchomvu na Dj Fetty.
Hawa jamaa mwanzo walikuwa wakibishana kuhusu mauzo ya CD na wauzaji feki sasa baada ya ubishani wa muda  ndipo B12 ambaye ni host wa kipindi akaamua kuzima mic, halafu Fetty akaiwasha bila ya wao kujua na kuendelea na ugomvi wa kabali, mangumi na purukushani kibao ndani ya studio hizo mpaka Soudy Brown (Gossip Cop) alipookoa jahazi baada ya kuingia studio na kuwapa taarifa kuwa hawakuwa wamezima mic, so kiufupi upuuzi wote ulikwenda hewani!!!! Sikiliza mwenyewe hapa jinsi hali ilivyokuwa...Hatari sana!

1 comments:

  1. hahahahaaaaaa!!!!! ka Fetty sijui ndo kalikabwa!!!! poleni aiseee

    JibuFuta