Siku kama ya leo miaka 26 iliyopita ndege ya abiria aina ya Airbus ya
shirika la ndege ya Iran iliyokuwa ikitoka Bandar Abbas kusini mwa Iran
na kuelekea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, ilishambuliwa kwa
makombora mawili ya jeshi la Marekani kwenye maji ya Ghuba ya Uajemi.
Manowari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes ilifyatua makombora hayo
na kuua watu wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo. Shambulio
hilo lilidhihirisha zaidi unyama wa serikali ya Marekani.
Viongozi wa
Marekani walizidisha ukatili wao pale walipomzawadia medali ya ushujaa
nahodha wa meli hiyo kutokana na kitendo hicho kilichoonekana na
serikali ya Washington kuwa eti ni cha kishujaa.
0 comments:
Chapisha Maoni