Msanii nguli katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt
Ezekiel (pichani) anadaiwa kuanza kusaka mtoto ikiwa ni miaka miwili
tangu afunge ndoa na Sunday Dimonte.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa
Aunt, siku si nyingi staa huyo atakwenda kuweka makazi ya muda kwa
mumewe Dubai hadi atakapopata ujauzito.
Akizungumza rafiki huyo ambaye aliomba jina
lake lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ‘matarumbeta’, alisema wengi
wanadai mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu
hicho hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa
ujauzito.
Kama mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo. Lakini baadaye ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai
alisema rafiki huyo.
Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai, muda si mrefu ataondoka.
Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai, muda si mrefu ataondoka.
Nadhani unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia afya njema ni muhimu ndoa ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai ndiyo mipango yangu.
Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume wangu amefungwa! Sitaki kuwajibu kwa maneno, nataka kuwajibu kwa vitendo
alitamba Aunt.
0 comments:
Chapisha Maoni