Jumatatu, Julai 28, 2014

MZINDAKAYA ANYANG'ANYWA NYUMBA 12

WIZARA ya Ujenzi imeinyang’anya Kampuni ya Agriculture and Animal Food Industries Ltd (Saafi), inayomilikiwa na mwekezaji mzalendo na mwanasiasa mkongwe, Dk. Chrisant Mzindakaya nyumba 12 za umma ambazo ilikuwa imezipanga kibiashara kwa miaka 12.
Nyumba hizo 11 za kuishi na moja ofisi zilizojengwa na Shirika la Maendeleo la Norway mwaka 1988,  zimekabidhiwa rasmi Juni 17 mwaka huu, kwa Wakala wa Majengo (TBA), mkoani hapa na Wizara ya Ujenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi huo wa serikali baada ya kukagua nyumba hizo juzi, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly (CCM), alisema ana furaha kwani nyumba hizo zilikuwa zikimnyima usingizi kutokana na maofisa serikalini wakiwemo majaji na baadhi ya wakuu wa idara kuishi nyumba za kupanga, lakini sasa wataishi nyumba hizo ambazo ni bora na zenye usalama wa kutosha.
Alibainisha kuwa baada ya kutembelea nyumba hizo na kuzikagua akiongozana na Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Rukwa, Deocles Kalikawe, amebaini kuwepo kwa upungufu mkubwa ambao alidai mwekezaji aliyezipanga kibiashara atalipia gharama zote za ukarabati.

0 comments:

Chapisha Maoni