Polisi nchini China wamemkamata mtu asiyekuwa na mikono akiendesha gari.
Bwana huyo Wo Guo (45) si tu kwamba hakuwa na leseni bali alikuwa
akitumia mguu wake wa kulia kubadili gia huku mguu wa kushoto ukikanyaga
mafuta na breki.
Msemaji wa polisi amesema:
Msemaji wa polisi amesema:
Ni jambo la ajabu, lakini ni hatari sana kwake kuendesha gari.
Polisi huyo amesema itakuwa
vyema kama ataajiri dereva wa kumuendesha. Gari la bwana Wo
linashikiliwa na polisi ili kumzuia asiendelee kuendesha.






0 comments:
Chapisha Maoni