Ijumaa, Julai 25, 2014

MKE WA MBUNGE WA CCM AUA HOUSE GIRL WAKE

Mfanyakazi wa ndani wa mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Ciril Chami (CCM) aitwaye Mariam Said (16) amefariki dunia mapema alfajiri ya leo ikiaminika kwamba kifo chake kimesababishwa na kipigo toka kwa mke wa Mbunge Chami, sababu kubwa ikielezwa kuwa binti huyo ambaye ni muislamu alikataa kata kata kwenda kuhudhuria misa kanisani.
Msimamo wa binti huyo ulimpelekea kipigo kikali, na hata mashuhuda walioshuhudia kipigo hicho cha kikatili kwa huyo binti, mke wa Mbunge inasemekana aliwajibu kwa lugha ya kejeli na kuwaambia hakuna mtu anaweza kumfanya chochote hata akimwua, kwani serikali ni yao, na CCM ndiyo inayoongoza dola, kwamba mahakama yetu, polisi wa kwetu, hakuna kima atakayenigusa. Alifoka mke wa Chami.

0 comments:

Chapisha Maoni