KESI ya kubaka inayomkabili mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha,
Emmanuel Mbasha (32), inatarajiwa kusikilizwa Agosti 22, mwaka huu,
baada ya upelelezi kukamilika.
Hatua hiyo inakuja baada ya mshitakiwa huyo jana kusomewa maelezo ya
awali ya kesi hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Akimsomea maelezo hayo jana mbele ya Hakimu Wilberforce Luago, Wakili
wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai Mei 23 mwaka huu, eneo la
Tabata-Kimanga, mshitakiwa alimbaka shemeji yake wakati mkewe, Flora
akiwa hayupo nyumbani.
Mbasha, alikiri siku hiyo mkewe kutokuwapo nyumbani, lakini hakumbaka shemeji yake kama inavyodaiwa.
Wakili huyo wa serikali, alidai Mei 25, mwaka huu, Mbasha alimbaka
tena shemeji yake ndani ya gari, wakati wanakwenda kumtafuta Flora
alipo, tuhuma ambazo alizikana pia.
Alidai siku hiyo hiyo, binti huyo alikwenda kutoa taarifa polisi na
kupewa PF 3 na kwenda Hospitali ya Amana; kwamba daktari alithibitisha
binti huyo aliingiliwa kimwili.
Baada ya Katuga kusoma maelezo ya awali, aliiambia mahakama kuwa watakuwa na mashahidi wanne.
0 comments:
Chapisha Maoni