Malkia Elizabeth wa Uingereza usiku wa kuamkia hii leo
alifungua michuano ya 20 ya jumuia ya madola ambayo kwa mwaka huu
inafanyika mjini Glasgow nchini Scotlnd.
Malkia Elizabeth, alifungua rasmi michuano hiyo kwa kuusoma ujumbe
wake uliokuwa umehifadhiwa katika kile kinachofahamika kama The
Commonwealth baton yaani mwenge wa jumuiya ya madola.
Maelfu ya wanamichezo kutoka nchi 71 wameshiriki katika ufunguzi huo
mbele ya watu elfu 40 waliokuwa uwanjani, huku shamra shamra za ufunguzi
huo zikifuatiliwa na mashabiki wengine duniani kupitia vyombo vya
habari.
Hali ya hewa katika mji wa Glasgow inapofanyika michuano hiyo, katika
kipindi hiki imetambulishwa rasmi kuwa ndiyo yenye joto zaidi kwa mwaka
huu baada ya kufikia nyuzi joto 25.
Michuano ya Jumuia ya Madola kwa mwaka 2014, itahusisha michezo 17 kwa siku 11.
Michuano ya jumuiya ya madola uhusisha nchi zilizowahi kuwa chini ya utawala wa himaya ya Uingereza.
0 comments:
Chapisha Maoni