Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika
maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia
katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea
janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya
kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira
magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo
yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra
yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia
katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo
katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na
janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale
kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea
nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo
hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.
0 comments:
Chapisha Maoni