Tafiti zinaonesha kuna idadi kubwa ya watu wanaotumia
Facebook hubofya zaidi picha au video zinazoonesha matukio yanayoendana
na ngono ama picha chafu. Lakini imebainika kuwa baadhi ya video hizo
hutumiwa na hackers kuweza kuaccess taarifa za mtumiaji na kuteka
akaunti yake.
Wataalamu wa masuala ya mitandao wa Uingereza wamewatahadharisha
watumiaji wa Facebook na kuwataka kuwa makini na video zinazosambaa
zikionesha msichana au mwanamke (hata kama wanamfahamu) akiwa anavua
nguo na kuonesha kuwa ukibofya itakupeleka Youtube kuangalia video
nzima.
Wameeleza kuwa video hizo hutuma taarifa zisizotegemewa kwenye
browsers kwenda kwenye flash player na kisha kuiba taarifa za siri za
mtumiaji.
0 comments:
Chapisha Maoni