Alhamisi, Julai 24, 2014

BAADA YA KUJIFANYA ASKARI, MWANDISHI WA HABARI NA USALAMA WA TAIFA AKAMATWA NA POLISI

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikiria kijana mmoja akituhumiwa kujifanya mwandishi wa habari, askali wa jeshi la polisi, na usalama wa taifa, huku akikana kitambulisho chake ambacho kina picha yake akidai kuwa alikuwa akikipeleka polisi kutokana na kukiokota.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Acp Suzan Kaganda amemtaja mutuhumiwa wa utapeli huo kwa jina la Mussa Mbeko,( 24)  ambapo amewataka wananchi ambao watakuwa wameishatapeliwa au kufanyiwa kazi yoyote inayohusiana na uhaskali na mtuhumiwa huyo kufika katika kituo cha polisi kutoa taarifa hizo.
Wakati huo huo kamanda wa polisi Suzani Kaganda kwa niaba ya mkuu wa polisi nchini amemzawadia kiasi cha shilingi elfu 90,000/- kama zawadi askali mkaguzi wa polisi Harun Kasubi, baada ya kukataa kupokea rushwa ya thamani hiyo hiyo kutoka kwa vijana waliokuwa wakivuta madawa ya kulevya aina ya eloin, huko katikka nyumba ya kulala wageni Kenios Isevya mjini Tabora.

0 comments:

Chapisha Maoni