Ikiwa dirisha la usajili limeshafunguliwa tangu wiki iliyopita kwa
timu mbali mbali kuanza kufanya usajili wa wachezaji na zingine zikianza
mazoezi, timu ya Young Africans imeweza kuweka wazi majina ya awali ya
baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia katika msimu ujao wa 2014/2015.
Young Africans ambayo msimu uliopita ilikua na kikosi bora kabisa
ambacho kiliweza kuwatoa jasho Mabingwa wa Kihistoria Barani Afrika timu
ya Natioal Al Ahly katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, ambapo
Mabingwa hao wa kutoka nchini Misri waliweza kusonga mbele kwa mikwaju
ya penati.
Msimu uliopita Young Africans ilikuwa na kikosi cha
wachezaji 30 kutoka timu ya Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu
ya vijana (U20) waliokuwa wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na
kuingozea nguvu timu ya wakubwa katika michezo mbalimbali.
Kutokana
na ripoti ya Benchi la Ufundi iliyowasilishwa mara baada ya kumalizika
kwa Msimu wa Ligi Kuu 2013/2014 baadhi ya wachezaji hawataitumikia tena
Yanga SC kwenye msimu ujao, wachezaji 11 wamemaliza muda wao na
kumalizana na uongozi hivyo wapo huru kujiunga vilabu mbalimbali:
Wachezaji hao ni:
1. David Luhende
2. Athuman Idd "Chuji"
3. Geroge Banda -U20
4. Yusuph Abdul -U20
5. Rehani Kibingu -U20
6. Hamisi Thabiti
7. Reliants Lusajo
8. Bakari Masoud - U20
9. Shaban Kondo
10. Abdalllah Mguhi "Messi" U-20
11. Ibrahim Job
Hii
ni orodha ya awali ya wachezaji ambao hawataitumikia Yanga SC msimu
ujao, huku zoezi la usajili likiendelea kujaza baadhi ya nafasi zilizopo
kulingana na maelekezo ya Benchi la Ufundi.
0 comments:
Chapisha Maoni