Kuna taarifa kuwa watu ishirini wameuawa katika shambulio kwenye kijiji Mashariki Kaskazini mwa Kenya.
Mwandishi wa habari anasema watu wenye silaha walivamia kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya jumapili.
Mwandishi wa habari anasema watu wenye silaha walivamia kijiji cha Gunana katika County ya Wajir mapema siku ya jumapili.
Amesema mapigano yalizuka kutoka na mgogoro baina ya koo mbili za Degodia na Gare.
Ni mzozo wa mpaka baina ya koo hizo ambao wakuu wanautambua, lakini bado hawakuweza kuupatia ufumbuzi.
Aidha mwandishi wa BBC ameongeza kuwa pamoja na
kwamba kuliwahi kutokea mapigano mengine hapo awali lakini hayajawahi
kusababisha vifo vya watu wengi kwa mara moja kama ilivyotokea siku ya
jumapili.
Mauaji haya yanakuja wiki moja baada ya watu
wapatao 60 kuuwawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea eneo la
Mpeketoni katika pwani ya Kenya lililodaiwa kufanywa na wapiganaji wa Al
Shabaab .
Wapiganaji hao walivamia vijiji viwili karibu na
mji wa Mpeketoni, na kufanya mashambulizi ambapo katika la kwanza
lilisababisha mauaji ya wau 48 na baadae la pili liliua watu wapatao 20.
0 comments:
Chapisha Maoni