Wakichangia mjadala wa mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa taifa na
makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2014/15, mbunge wa
Ludewa Mhe Deo Filikunjombe amesema wabunge wanapata mishahara,masurufu
na posho ambazo ni kubwa lakini hawalipi kodi huku mbunge Mhe. Lugola
akisisitiza mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa-brn- ni sehemu
ya michepuko inayokwamisha bajeti.
Aidha kwa upande mwingine baadhi ya wabunge
wamewataka wabunge kujitadhimini kama wanalipa kodi za nyumba ili wawe
mfano badala ya kuwasinikiza wananchi kulipa kodi ya nyumba wakati wao
hawalipi na kusisitiza sekta ya nyumba nchni inaweza kuiiingizia
serikali zaidi ya trilioni moja kwa mwaka.
Kwa mujibu wa kalenda ya serikali inaonyesha
zimebaki takribani siku kumi kukamilika mwaka wa fedha wa serikali wa
2013/2014 ambapo baadhi ya wabunge wameendelea kulalamikia kutokamilika
kwa fedha za miradi ya maendeleo iliyotajwa katika mwaka husika.
0 comments:
Chapisha Maoni