Uingereza wameondolewa kutoka kombe la dunia la mwaka
huu huko Brazil baada ya raundi ya kwanza, kwa mara ya kwanza tangu
mwaka 1958.
Uingereza ilibanduliwa baada ya Italia kupoteza mechi yao dhidi ya Costa Rica 1-0 huko Recife katika kundi D.
Uingereza ilikuwa imeshindwa na Uruguay na Italia katika mechi zilizotangulia.
Uingereza ilihitaji Italia kushinda mechi yao
ili wapate matumaini ya kuendelea lakini Costa Rica walipoishinda
Italia, matumaini yao yakapotea pia.
Kikosi cha Uingereza kiliitazama mechi hiyo kutoka katika makazi yao, hotelini huko Rio.
Aliyekuwa mlinzi katika kikosi hicho, Rio
Ferdinand anaamini kuwa kukosa uzoefu kulichangia pakubwa katika
kuondolewa kwa timu hiyo mapema hivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni