MAHAKAMA ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, jana imewaachia huru
viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja
na washitakiwa wengine 21 waliokuwa wakikabiliwa na kesi tatu tofauti
za kufanya maandamano bila kibali.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Halfani Ulaya, aliwaachia huru
viongozi hao ambao ni Kaimu Mwenyekiti wa Mkoa, Kasim Ahmad Bingwe,
Katibu wa Wilaya, Fidelis Vitus Mlaponi na Katibu wa Jimbo, Musa
Mustafa Mwadewa pamoja na washitakiwa wengine 13 ambao aliwaona hawana
hatia katika kesi namba 263 ya 2013.
Akizungumza na Fichuo TZ baada ya kesi hiyo jana, wakili
aliyepelekwa Masasi na CHADEMA ili kuwatetea viongozi hao, Nyaronyo
Mwita Kicheere, alisema Bingwe, Mlaponi na Mwadewa pamoja na wenzao 13
walikuwa wanakabiliwa na makosa ya kuandamana bila kibali, kuchoma moto
nyumba na kuharibu mali ya Mbunge wa Masasi, Mariamu Kasembe (CCM).
0 comments:
Chapisha Maoni