Mlipuko umeripotiwa kutokea katika taasisi moja ya
umma ya mafunzo ya afya katika mji wa Kano ambao ni wa pili kwa ukubwa
nchini Nigeria.
Duru zinasema kuwa idadi ya watu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo dhidi ya kituo cha mafunzo ya afya , bado haijulikani.
Mji huo umewahi kulengwa na wapiganaji wa
kiisilamu wa Boko Haram, ambao wanataka kubuniwe taifa la kiisilamu
Kaskazini mwa Nigeria.
Majimbo matatu Kaskazini mwa Nigeria bado yapo
chini ya sheria ya hali ya hatari kufuatia miaka mingi ya harakati za
wapiganaji hao wa kiisilamu.
0 comments:
Chapisha Maoni