Afisa mmoja ameiambia amesema kwamba wafungwa wasiopungua
250 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walitoroka gerezani majira
ya alfajiri.
Afisa huyo anayehudumu katika afisi ya gavana
iliyoko kusini mwa Kivu alisema kuwa watu watatu waliaga dunia, akiwemo
mlinzi aliyeshindwa kuwakabili wafungwa hao walipokuwa wakitoroka.
Polisi wameshika doria Bukavu,jiji ambalo limejengwa kandokando ya ufuo wa ziwa Kivu mashariki mwa Kongo ili kuwasaka.
Mkazi mmoja amesema kwamba watu waliojawa na hofu walikuwa wakijificha katika nyumba zao.
Mwanahabari wa BBC Maud Jullien, anasema kuwa
kutoroka gerezani imekuwa jambo la kawaida nchini humo – wafungwa
wapatao 240 walitoroka katika mji mwingine wa Mashariki ya taifa hilo
chini ya mwaka mmoja uliopita.
Afisa mmoja wa polisi ameliambia shirika la AFP
kwamba walinzi wa magereza walishindwa kukabiliana n awafungwa hao ambao
walichukua silaha na kuharibu milango ya magereza.
Wakazi wanasema milio ya risasi ilisikika asubuhi hiyo jijini.
Wanaharakati wa vyama vya raiya wanasema kuwa
huenda idadi ya waliotoroka ikawa zaidi, kwani idadi jumla ya wafungwa
waliokuwemo gerezani ni 1,500 huku maafisa husika wakikisia kuwa zaidi
ya asilimia 80 ya wafungwa walikuwa wametoroka.
Magereza nchini Kongo mara nyingi huwa na idadi kubwa kupita kiasi na hali ya maisha huwa mbovu kwa wafungwa.
0 comments:
Chapisha Maoni