Cesc Fabregas amekamilisha rasmi taratibu za kuhamia Chelsea huku
klabu yake ya zamani Arsenal ikiamua kutokutumia kifungu cha kumrudisha
kwa maelekezo ya meneja wa klabu hiyo kua haitajiki Emirates kwa salsa.
Inaaminika kwamba Barcelona imepokea £30million kutoka Chelsea kama ada
ya kiungo huyo mwenye miaka 27 na kuingia mkataba wa miaka mitano na
Fabregas kutumikia klabu hiyo ya Stamford Bridge.
Inaaminika maamuzi ya Fabregas yamekuja baada ya kuona jitihada za
Chelsea kumfuata mpaka Brazil aliko sasa na timu yake ya taifa Spain
huku klabu ya Arsenal ambayo kama ingemtaka isingeuzwa klabu nyingine
yoyote zaidi ya hiyo kutokuonesha kumtaka.
0 comments:
Chapisha Maoni