Wasimamizi wa kimataifa wametoa ripoti kuhusiana na mapigano
yaliyojiri kati ya askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda.
Timu ya wachunguzi wa mipaka katika eneo la Maziwa Makuu baada ya
kufanya uchunguzi wametoa ripoti iliyoeleza kuwa, kinyume na madai ya
Rwanda mapigano hayo yalijiri katika miinuko ambayo ipo katika ardhi ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Timu hiyo iliyojumuisha wawakilishi
kutoka nchi 10 duniani imesema kwenye ripoti yake hiyo kuwa, katika
mapigano hayo imeonekana kuwa, askari watano wa Kongo walipigwa risasi
kichwani. Hii ni katika hali ambayo maafisa wa Kongo wanadai kwamba
wahanga hao walinyongwa huku Rwanda ikidai kwamba askari hao waliuawa
baada ya kuingia katika ardhi yake.
Katika ripoti hiyo nchi mbili hizo jirani zimetakiwa kuepuka
kupeleka askari kwenye miinuko hiyo yenye kuzozaniwa ili kuepusha
kukaririwa tukio kama hilo. Pia tume hiyo ya wasimamizi wa kimataifa
imetaka kuitishwa haraka mkutano wa viongozi wa nchi mbili hizo ili
kutatua hitilafu zao.
0 comments:
Chapisha Maoni