Wanaume saba wamekamatwa nchini Misri, baada ya
kushukiwa kuwadhulumu kiongono wanawake katika sherehe za Jumamosi za
kumkabidhi rasmi mamlaka Rais Abdul Fattah al Sisi.
Hatua ya kuwakamata wanaume hao, inakuja baada
ya kanda ya video kusambazwa kwenye internet ikionyesha mwanamke
akivuliwa nguo na kuvamiwa na genge la wanaume
Haijulikani ikiwa kanda hiyo ilinaswa, lakini
walioshuhudia kitendo hicho waliambia BBC kwambwa unyama huo ulitokea
Jumapili usiku.
Wiki jana maafisa wa utawala nchini Misri,
waliharamisha dhuluma za kingono na kuufanya uhalifu kwa mara ya kwanza
adhabu yake ikiwa miaka mitano jela kwa watakaopatikana na hatia.
0 comments:
Chapisha Maoni