Mwanasheria wa mwanamke wa Sudan aliyekamatwa siku
chache baada ya kuachiwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa kuasi dini ya
Kiislam kwa kuolewa na Mkristo, amesema mteja wake anatuhumiwa kwa
kughushi nyaraka za safari.
Amesema mwanamke huyo Meriam Ibrahim bado anashikiliwa katika kituo cha polisi katika mji Mkuu wa Khartoum.
Sudan Kusini ambayo ndio iliyompa
nyaraka hizo imesema kuwa nyaraka hizo ni halali kwa vile ameolewa na
mwanaume raia halisi wa Sudan Kusini.
Mwanasheria wa Meriam Ibrahim amesema yeye
pamoja na mumewe walikuwa wakiohojiwa kuhusuana na hati za kusafiria.
Ilikuwa inasadikiwa kuwa walikuwa wanasafiri kuelekea nchini Marekani.
Awali Marekani ilisema itashirikana na Sudan
kuhakikisha kuwa mwanamke aliyesamehewa hukumu ya kifo kwa kuasi dini ya
Kiislam anaruhusiwa kuondoka nchini humo baada ya kukamatwa katika
uwanja wa ndege wa Khartoum.
Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alihukumiwa kifo
kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu
alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
Watu waliomkata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika kuwa wanajeshi wa serikali.
Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu
arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya
kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa.
Alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela punde baada ya kuhukumiwa.
Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.
Kabla ya kuzuiliwa kwaketena, jamii ya kimataifa yalipongeza uamuzi wa kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake.
0 comments:
Chapisha Maoni