Ufalme wa kitamaduni wa Tooro nchini Uganda, umemtaka
Rais wa Uganda Yoweri Museveni kumuomba msamaha mfalme wao na kuondoa
matamshi yake ambapo alimuita mfalme huyo mtoto.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Uganda la The observer.
Jarida hilo liliripoti kuwa waziri
mkuu wa ufalme wa Tooro, Minister Steven Kaliba, alionya ikiwa Rais
Museveni hatoomba msamaha matokeo yake yatakuwa mabaya.
Hata hivyo waziri huyo amekanusha madai hayo.
Mfalme wa Tooro ana umri wa miaka 22 pekee na
anajulikana kama Omukama Oyo. Rais Museveni alimuita mfalme huyo
'Akavuka ke Tooro' ikitafsiriwa kwa kiengereza kama kusema 'Kijana huyu
wa Tooro.
Jarida la Observer limedai kuwa mfalme huyo
anatishia kususia chakula kutokana na kile anachosema ni njama ya Rais
Museveni kuvunja ufalme wa Tooro.
Ufalme hata hivyo, umekanusha
madai hayo katika taarifa yake ukisema kuwa Mfalme huyo atafunga kula
mwezi ujao kwa sababu za kitamaduni na kidini.
Ufame umesema kuwa sio mara ya kwanza kwa mfalme
wa Tooro na familia yake kufunga kukula , ukisema kuwa wao hufanya
hivyo kila mwaka akitaka kumuomba Mungu kumpa mwongozo katika utawala
wake.
Kadhalika ufalme huo umekana kuwa mfalme anafunga kukula kwa sababu ya matatizo ambayo ufalme huo unakumbwa nayo.
Ufalme huo umesema kuwa umekasirishwa sana na
matamshi ya Rais Museveni kumuita mfalme kama kijana ukisisitiza kuwa
umri, rangi na muonekanao wa mfalme Oyo Nyimba Kabamba sio wa
kuzungumziwa hadharani.
Licha ya kwamba kila mtu anaweza kutoa maoni
yake kuhusu swala lolote, ufalme umetaka kumjulisha Museveni kuwa mfalme
huyo ni fahari ya watu wa Tooro na kwamba awe mtoto au mtu mzima
anajulikana tu kama mfalme.
Umemtaka Rais Museveni kukumbuka kuwa yeye ni mlinzi na kiongozi anayepaswa kutunzwa na jamii
0 comments:
Chapisha Maoni