BAADA ya pweza Paul aliyekuwa akiishi Ujerumani kujizolea umaarufu
wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini,
fainali za mwaka huu nchini Brazil ameibuka mtabiri mwingine aitwaye
Cabeção au Big Head.
Big Head ambaye ni kasa mwenye umri wa miaka
25, anayeishi katika kijiji cha Praia Do Forte nchini Brazil
ameitabiria nchi yake ya Brazil kuibuka na ushindi katika mechi ya
ufunguzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Croatia kesho.
Big Head ameanza kazi yake hiyo jana, Jumanne kwa kutabiri mechi ya
ufunguzi kati ya Brazil na Croatia. Kasa huyo anafanya utabiri kwa
kuchagua vyakula. Alichagua mmoja wa samaki waliokuwa wananing'inia
katika bendera za Brazil, Croatia na kwenye mpira.
0 comments:
Chapisha Maoni