Jumanne, Juni 03, 2014

KOMBA ADAI UMEME WAKE KWA WAZIRI MASELE BAADA YA KULA UGALI WAKE

Mbunge wa Mbinga‬ Magharibi, John Komba‬ ametoa mpya bungeni alipomtaka Naibu Waziri wa Nishati na Madini ampe umeme kwa kuwa amekula ugali wake.
Komba alitoa kauli hiyo wakati akichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2014/15.
Wewe Mheshimiwa (Naibu Waziri wa Nishati, Stephen) Masele ulifika nyumbani kwangu Nyasa na mke wangu akakusongea ugali, tukala wote lakini leo umenisahau
 alilalamika Komba.

0 comments:

Chapisha Maoni