Jumatatu, Juni 09, 2014

KAHAWA NI NZURI, TUMIA...LAKINI KUWA MAKINI

Ukinywa kahawa wakati umechoka, baada ya dakika tano uchovu wote huisha. Ila, unatakiwa unywe kahawa kwa  nadra kwa kuwa kahawa pamoja na vinywaji vyote vyenye ‘Caffeine’ ni ulevi ambao ukiuendekeza huweza kuwa ‘teja’ wa vinywaji hivyo (addicted).

Kahawa ndiyo yenye kiwango kikubwa cha ‘Caffeine’ kuliko vinywaji vingine vyote. ‘Caffeine’ hupatikana pia katika chocolate, chai, vinywaji vyote vyenye neno ‘Cola’ na wakati mwingine utaipata kwenye dawa kama vile ‘Excedrin’ na ‘Anacin’ pia.
‘Caffeine’ humsisimua mnywaji kwa kumfanya ajione ni mwenye nguvu, makini na wakati mwingine hujiona mwenye furaha. Hii hutokana na ‘Caffeine’ kuichachua mishipa ya fahamu na misuli ya mwili yaani ‘Nervous System’ na hata ‘Adrenal Gland’. Hata hivyo, wataalamu wa afya wanasisitiza kuinywa kahawa na vinywaji vyote vyenye caffeine kwa nadra na wenye matatizo ya moyo wasinywe kabisa kwa kuwa ‘caffeine’ hupandisha mapigo ya moyo.
Caffeine inapoingia mwilini kama binadamu anavyoliogopa giza na ndivyo mwili huviogopa vyakula vyeusi ambavyo vyote ni ‘antioxidants’, yaani vinanyotoa sumu mwilini haraka kwa kuwa mesenja wa ubongo (neurotransimiter) huuambia ubongo kuwa mwilini kumeingia sumu na hivyo ubongo hutoa sukari yote ya akiba ili ikasaidie kutoa sumu hizo na ndipo mywaji hujikuta akitokwa na jasho.
Unywaji wa kahawa na soda, chocolate n.k, huvifanya viungo vya mwili hasa mifupa, misuli na mishipa ya fahamu kuchoka haraka. Viungo hivi vikichoka kinga ya mwili nayo pia hushuka na maradhi ya mara kwa mara huanza.

Nina uhakika pia kuwa wapo wasomaji ambao wanasoma makala haya huku wameegemea viti vyao kwa kuwa mgongo, kiuno na magoti vyote vinauma sana, misuli na mishipa imekakamaa. Unywaji wa vinywaji vyenye caffeine kwa wingi huchangia hali hiyo kwa kiwango kikubwa sana.
Hali huwa mbaya katika ‘uteja’ wa caffeine ambapo kiwango cha lehemu hupanda na vitamin B za aina karibu zote pamoja na aina nyingi tu za madini hupotea mwilini. Japo siyo wengi, ila wapo baadhi ya wanawake ‘mateja’ wa caffeine ambao wameripotiwa kuwa na maradhi ya matiti na uzazi.
Hizi ni zama za sayansi na teknolojia ambayo imeyafanya makazi ya wengi wetu kuwa mijini. Mijini kunywa kahawa, soda, chai, na caffeine nyinginezo imekuwa ndiyo mila na desturi.
Hii ndiyo sababu maradhi ya viungo yanaripotiwa zaidi maeneo ya mijini kuliko vijijini na angalizo ni kuwa makini na ‘ofa’ za vinywaji hivyo vya bure ambavyo vinaweza kuugharimu urefu wa maisha yako ambayo ni ghali kuliko kitu chochote.
Kumbuka, kunywa kahawa au chai kwa kiwango kidogo, mfano kikombe kimoja kwa siku au hata robo kikombe inatosha.
Inashauriwa kama unapenda chai, tumia ‘Green Tea’ au chai ya kijani badala ‘Black Tea’ au chai nyeusi, kwa wenye maradhi ya moyo wanashauriwa kutokunywa kahawa kabisa.

0 comments:

Chapisha Maoni