Jumatatu, Juni 02, 2014

JUSTIN BIEBER AOMBA RADHI KWA UBAGUZI

Mwanamuziki maarufu duniani Justin Bieber, ameoamba radhi kwa kutumia neno la kibaguzi wakati akiwakejeli wamarekani weusi kuhusu swala la ubaguzi wa rangi.
Bieber alitumia neno hilo N***** katika kikao na marafiki zake alipokuwa anafanya vichekesho kuhusu swala la ubaguzi wa rangi.
Kanda ya video ya Bieber akitamka neno hilo, iliwekwa kwenye mtandao wa The Sun Jumapili.
Jarida hilo linadai kuwa marafiki za Bieber wamekuwa na ufahamu kuhusu kanda hiyo na wamekuwa wakitumia pesa kujaribu kuificha.
Katika kanda hiyo Bieber anasikika akiuliza kwa nini wamarekani weusi wanaogopa misumeno inayotumia nishati.
Kanda hiyo inamalizika kwa Bieber kukejeli wamarekani wausi kwa kutoa sauti ya msumeno na kisha kurejelea kauli hiyo ya ''Kimbia N*****'' mara tano.
Hata hivyo inasemekana kanda hiyo ilirekodiwa kama sehemu ya makala maalum kumhusu msanii huyo.

0 comments:

Chapisha Maoni