HOFU ya siasa za kuchafuana kuelekea katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwakani imeanza kushika kasi miongoni mwa wabunge
ambao tayari wameanza kuanikwa picha zao kwenye mitandao ya kijamii
wakiwa faragha.
Fichuo TZ imedokezwa kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa
wakifadhili upigaji wa picha za video na mnato kwa kuwatumia wahudumu
wa hoteli mbalimbali za ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma, kunakofanyika
vikao vya Bunge.
Inaelezwa kuwa lengo la kufadhili mikakati hiyo ni kuwaharibia majina
wabunge husika ili wasipate fursa ya kuaminika kwenye jamii, hivyo
kunyimwa kura katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu mwakani.
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa kutokana na kukua kwa
teknolojia ya habari na mawasiliano, baadhi ya wataalamu wa masuala ya
mitandao wamekuwa wakitengeneza picha za ngono kwa lengo la kujipatia
fedha kwa njia zisizo halali.
Inadaiwa baadhi ya watu huwasiliana na wahusika juu ya picha hizo
huku wakiwatishia kuwa endapo wasipowapa fedha watazitoa kwenye jamii.
Tayari picha za Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba (CCM) na
Ukerewe, Salvatory Macheli (CHADEMA), zimetolewa zikiwaonyesha wakiwa
faragha.
Komba, alikaririwa na vyombo vya habari kuwa baadhi ya watu wamekuwa
wakitumia teknolojia kutengeneza picha hizo kwa malengo ya uovu.
0 comments:
Chapisha Maoni