Ijumaa, Juni 06, 2014

AZAM FC KUWEKA KAMBI HISPANIA

KATIKA kuhakikisha wanafanya vyema kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na michuano ya kimataifa, Klabu ya Azam inatarajia kuweka kambi nchini Hispania ikiwa ni sehemu ya maandalizi.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu, wanatarajia kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kilisema kuwa, klabu hiyo imepanga kuweka kambi yake nchini humo kwa lengo la kulinda heshima mara baada ya kutwaa ubingwa wa ligi.
Aidha, kilisema kocha wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog, anatarajia kurejea kati ya Juni 13, mwaka huu huku kambi ikianza Juni 16.
Kambi imepangwa kuwa Hispania, lengo likiwa ni kuwapa nafasi wachezaji kujifunza vitu vingi kama ambavyo inajulikana nchi hiyo kwa soka la uhakika, pia mwalimu anaweza kutua Dar kati ya Juni 13 
kilisema chanzo hicho.
Idrissa Nassor alihojiwa kuhusiana na ishu hiyo ambapo alisema:
Klabu imempa jukumu kocha Omog aamue yeye kambi anataka iwekwe wapi kwa kuwa anajua wapi patamfaa

0 comments:

Chapisha Maoni