Jeshi la polisi Zanzibar limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa
mauaji ya askari wa polisi na mgambo mmoja ambao waliuwawa kwenye tukio
la uvamizi wa kituo cha polisi cha Kimanzimchana walaya ya mkuranga
mkoa wa Pwani Juni 11 mwaka huu.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda
wa polisi wa mkoa wa Kusini Pemba ACP Juma Yussuf Msige amemtaja
mtuhumiwa huyo kwa jina la Hamis Othman mzee maarufu kwa jina la Hamis
Mabunduki na makachero walifanikiwa baada ya kufuatilia nyendo zake na
kumkamata wakati wa mchana akiwa mafichoni katika kijiji cha Matale
Chake Chake Pemba na hivi sasa wanawasilaina nawenzao wa Pwani kwa ajili
ya upelelez i zaidi.
0 comments:
Chapisha Maoni