Algeria imefuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia.
The Desert Foxes walitoka nyuma bao moja kwa
nunge dhidi ya Urusi katika kipindi cha kwanza na kusawazisha na hivyo
kufuzu kama mshindi wa pili katika kundi H nyuma ya Ubeljiji
Hii ndiyo mara yao ya kwanza kupita mkondo wa kwanza. Algeria itaingia katika kumbukumbu za historia
ya Soka Afrika kuwa mwakilishi wa 6 kuwahi kufuzu kwa raundi hiyo ya 16
bora nyuma ya Cameroon Ghana Nigeria Morocco na Senegal .
Algeria
ilikuwa imefungwa mapema katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mkwaju
wake Aleksandr Kokorin aliyepata pasi murua kutoka kwa Dmitri Kombarov.
Hata hivyo vijana wa kocha Fabio Capello
walianza kulinda ngome yao mapema bila ya tahadhari kuwa baop lolote la
Algeria ingewarejesha nyumbani.
Mashambulizi ya Algeria yalizaa matunda kunako
dakika ya 60 Islam Slimani alipoisawazishia Algeria kutokana na mkwaju
wa freekick uliopigwa na Yacine Brahimi.
Wadau watachunguza tukio ambalo shabiki mmoja
anadaiwa kumulika kifaa cha Laser usoni mwa kipa wa Urusi Igor Akinfeev
kabla ya bao hilo la kusawazisha.
Kocha Capello amelalamikia hatua
ya refarii kupuuza tukio hilo akisema kuwa huenda marefarii wananjama
ya kuihujumu timu ya Urusi.
Urusi ilifanya mashambulizi kwenye lango la
Algeria la Algeria lakini wapi safu ya ulinzi ilikaa ngangari na
kuhimili mashambulizi hadi kipenga cha mwisho na hivyo kuipa Algeria
alama moja muhimu iliyoiwezesha kuweka historia ya kufuzu kwa raundi ya
pili ya kombe la dunia.
Algeria sasa imeratibiwa kukwaruzana na Ujerumani katika mechi ya 16 bora siku ya jumatatu.
0 comments:
Chapisha Maoni