Kikundi cha mashabiki wa muziki nchini Iran walioiga
wimbo maarufu wa mwanamuziki maarufu wa Marekani Pharrell Williams,
'Happy' wamejipata matatni baada ya kukamatwa na polisi.
Kanda ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.
Kanda ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.
Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa kanda ya video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa Iran
wamekamatwa katika miaka 35 iliyopita wakisherehekea na kujiburudisha
kwa mambo ambayo serikali inaona kama ya kukiuka maadili.
Hata hivyo vijana hao wanaosema ni waigizaji
wanadai kuwa walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa
wanatafuta waigizaji wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.
waliniambia kuwa wanatengeza filamu na kuwa walikuwa na kibali na ndio maana nikakubali kushiriki
alisema mmoja
wa vijana waliokamatwa.
Mtuhumiwa mwingine alisema walionasa kanda hiyo waliwaahidi kwamba hawataisambaza.
Kulingana na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, watu 13
walikamatwa kuhusiana na kanda hiyo, ingawa idadi kamili ya waliokamatwa
haijatangazwa rasmi.
Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo
wake huo mwaka huu ambao umekuwa maaruufu sana duniani, alielezea
kukasirishwa na hatua ya vijana hao kukamatwa.
alisema Pharrell katika ukurasa wake wa Facebook.
Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.
Polisi ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa
sheria ya mavazi inafuatwa, hushika doria mara kwa mara katika barabara
za mji mkuu Tehran.
Kanda hiyo ya "Happy we are from Tehran"
ilionekana kwenye mtandao wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia sasa
imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli serikali ya Iran wakisema kuwa Iran ni nchi ambako ni hatia kwa mtu kuwa na furaha.
Wimbo halisi wa Pharrell 'Happy' umepelekea
maelfu ya watu kote duniani kuiga video ya wimbo huo na kutengeza video
zao wenyewe. Kutoka Kenya, Marekani , Uingereza yaani nchi nyingi
duniani tu, watu wameiga video hiyo kwa kutengeza yao wenyewe.
0 comments:
Chapisha Maoni