Waziri wa Usalama wa Taifa wa Somalia amejiuzulu. Abdikarim
Hussein Guled amejiuzulu baada ya kujiri shambulio la kigaidi karibu na
bunge la Somalia mjini Mogadishu hapo jana. Taarifa zinasema kuwa, baada
ya shambulio hilo lililopelekea watu 10 kuuawa, waziri huyo wa usalama
wa Somalia alishinikizwa na wabungen ajiuzulu.
Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani
shambulio hilo lililofanywa na wanamgambo wa al Shabab kwenye jengo la
bunge la Somalia. Wajumbe wa Baraza la Usalama wamesema kuwa
wanasikitishwa na shambulio hilo dhidi ya bunge taasisi ambayo
inawakilisha wananchi wa Somalia, na ambako ni mahala wanapotumaini
kupata usalama, amani na maendeleo kwa njia halali.
0 comments:
Chapisha Maoni