Jumanne, Mei 27, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA MAY 28

Siku kama ya leo miaka 16 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 28 Mei 1998, kwa mara ya kwanza Pakistan ilianza kufanya majaribio matano ya makombora ya nyuklia. Majaribio hayo yalifanyika zikiwa zimepita wiki mbili tu, tokea mahasimu wao yaani India kufanya majaribio yao ya kombora la nyuklia. Baada ya hapo nchi hizo mbili zilikuwa zikipokezana katika kufanya majaribio yao ya makombora ya nyuklia. Amma cha kushangaza ni kuwa, majaribio ya nyuklia ya Pakistan yamekuwa yakizikasirisha mno nchi za Magharibi za Marekani na Ulaya, na kufikia hatua ya kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi.

Siku kama ya leo miaka 74 iliyopita inayosadifiana na tarehe 28 Mei 1940, Ubelgiji ambayo ilitangaza kutoegemea upande wowote mwanzoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, ilitekwa na majeshi ya Kinazi ya Ujerumani. Majeshi ya Ubelgiji ambayo yalikuwa yakipata usaidizi wa Uingereza, yalisimamisha vita kutokana na amri ya Mfalme Leopold wa Tatu, licha ya kusimama kidete kwa muda wa siku 18 dhidi ya majeshi ya Kinazi ya Ujerumani. Hatua hiyo ya mfalme Leopold, iliwakasirisha mno wananchi wa Ubelgiji na kuandaa mazingira ya kuondolewa kwake madarakani mwaka 1951.

0 comments:

Chapisha Maoni