Jumapili, Mei 18, 2014

TAHADHARI KUTOKA FACEBOOK NA TWITTER

Tahadhari zaidi zimetolewa nchini Kenya za kutokea mashambulio katika baadhi ya maeneo ya umma na foleni za barabarani.
Mitandao ya kijamii ya twitter na facebook imetumiwa kusambaza ujumbe miongoni mwa wananchi kutoa tahadhari hiyo.

Usalama umeimarishwa katika Ubalozi wa Marekani Kenya na ofisi za Umoja wa mataifa Nairobi, na hatua madhubuti zimechukuliwa kupunguza msongamano wa watu katika maeneo hayo.
Na huku hayo yakiarifiwa sekta ya utalii nchini humo imeendelea kupata hasara kubwa kutokana na kuondolewa kwa raia wa kigeni hasa Uingereza waliokuwa katika mji wa kitalii wa Mombasa kufuatia tishio la kulengwa katika shambulio.
Afisa Mkuu wa Shirika la kampuni linaloshughulikia utalii nchini, Kenya Tourism Federation, Agatha Juma anasema upungufu wa watalii nchini Kenya utasababisha ukosefu wa ajira, zaidi kwa raia wa Kenya wanaofanya katika hoteli mbali mbali nchini.
Kenya imeshuhudia mashambulio kadhaa katika siku za hivi karibuni katika maeneo mbali mbali nchini ukiwemo mji wa Mombasa na Nairobi, yaliosababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.

0 comments:

Chapisha Maoni