Ijumaa, Mei 02, 2014

SAFARI YA TRENI DAR ES SALAAM-MBEYA YAKWAMA KWA MUDA

Katika hali isiyokuwa kawaida train ya abiria ilokuwa imeanza safari yake saa nane kasoro mchana wa leo kutoka jijini kuelekea mkoani Mbeya imelazamika kugeuzia njiani kurudi pale kituoni TAZARA na itaendelea na safari saa kumi na moja na nusu jioni ya leo.
Sababu waloelezwa abiria inaitwa (SABABU ISIYOZUILIKA).Wote mlowasindikiza ndugu jamaa na marafiki jueni kwamba bado wapo hapa hapa jijini Dar mpaka sababu hiyo itapotengamaa.
Pia wadau msishangae siku utapoenda pale TAZARA kumpokea mgeni wako itakubidi ulipe kiingilio cha shiling elfu moja.

Kiasi hiki kipya kimepandishwa baada ya kile cha mia 5 cha awali.Kiwango hiki ni kikubwa sana kwa watu wa maisha ya chini wanaokuja kupokea ndugu zao.

0 comments:

Chapisha Maoni