Jumatatu, Mei 12, 2014

SABABU YA KUTOFANIKIWA VYAMA VYA USHIRIKA MKOANI NJOMBE

Ubunifu Mdogo wa Baadhi ya Viongozi wa Vyama Vya Ushirika Mkoani Njombe Katika Kuandaa Mipango Kazi na Kuandika Maandiko ya Miradi ni Miongoni Mwa Sababu Zinazochangia Vyama Hivyo Kushindwa Kuendelea na Wanachama Wake Kukata Tamaa.
Aidha Vyama Hivyo Pia Vimeonekana Kushindwa Kupiga Hatua za Kimaendeleo Kutokana na Wanachama Wake Kukosa Imani na Viongozi Wao Kwa Kukosa Ubunifu Katika Kuendesha Vyama Hivyo.
Akizungumza Wakati wa Semina ya Mradi wa Elimu ya Masafa Kutoka Makao Makuu ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Nchini Jijini Dar es Salaam Florian Haule Amesema Katika Mpango Huo wa Majaribio Kwa Mikoa Mitatu ya Njombe , Mbeya na Kagera Wanatoa Elimu Kwa Hiyo Kwa Maafisa na Viongozi wa Vyama Vya Ushirika Ili Kwendana na Wakati Uliopo na Namna ya Kufanikisha Kutoa Mikopo Yenye Riba Nafuu Kwa Wananchama Wake.
Wali Akizungumza Wakati wa Uzinduzi wa Semina Hiyo Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Thomas Nyamba Amesema Kuwa Wanachama Wengi Wamekuwa Wakikabiliwa na Riba Kubwa ya Mikopo Wanayokopo Kwenye Taasisi za Kifedha Hivyo Kupitia Vyama Hivyo Itawapa Nafuu Wanachama Kwa Kupata Mkopo Wenye Riba Ndogo.
Semina Hiyo Kwa Maafisa Ushirika na Viongozi wa Vyama Hivyo Imetolewa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika Nchini , Chini ya Ufadhili wa Serikali ya CANADA, Ambapo Vyama 25 Vya Ushirika Kwa Kila Wilaya Vinatarajiwa Kupatiwa Mafunzo Hayo na Vya 50 Vya Ushirika Kwa Mkoa Katika Mpango Huo wa Majaribio .

0 comments:

Chapisha Maoni