Je unamkumbuka mkalimani huyu aliyeuduwaza ulimwengu
kwa utafsiri wake wa ishara wakati wa mazishi ya hayati mzee Nelson
Mandela mwaka uliopita ?
Thamsanqa Jantjie aliyekashifiwa na ulimwengu
mzima na haswa walemavu kwa kutoa ishara zisizotafsirika kwa wale wenye
matatizo ya kusikia wakati wa mazishi ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini
Nelson Mandela sasa amepata ajira .
Jantjie alijitetea kuwa alishikwa na kiwewe na kuona mazingaombwe wakati wa maziko hayo.
Bwana huyo sasa ameonekana katika tangazo la biashara akikejeli tukio hilo lililompa umaarufu kote duniani.
Tangazo hilo la linapigia debe mtandao wa kijamii wa Livelens uliotengezwa na kampuni moja kutoka Tel Aviv Israili.
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Max
Bluvbland ameiambia BBC kuwa Jantjie yuko timamu na kuwa alitekeleza
majukumu yake bila tashwishi yeyote ''yeye ni mtu timamu aliyepatikana
na mkasa anaojutia.
Wataalamu wa lugha za ishara walisema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo.
Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta
Bogopane - Zulu alikanusha kuwa kulikuwa na suala la kukiuka taratibu
za kiusalama wakati mtafsiri huyo alionekana akisimama kwenye jukwaa
wakati wa ibada hiyo iliyokuwa ikitizamwa kote duniani na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali.
0 comments:
Chapisha Maoni