Wakati raia tisa wa China wakibainika kuugua ugonjwa wa dengue
na kulazwa hapa nchini, Rais Jakaya Kikwete amevunja ukimya na kuagiza
wizara zake mbili kukabiliana na ugonjwa huo kwa dharura.
Ugonjwa huo uliingia nchini tangu mwaka 2010
lakini mlipuko wake mkubwa ulibainika Machi mwaka huu na hadi jana
wagonjwa zaidi ya 400 walikuwa wameambukizwa, huku watatu wakiripotiwa
kufariki dunia, akiwamo Daktari Bingwa wa magonjwa ya akili, Dk Gilbert
Buberwa anayezikwa leo, Dar es Salaam.
Rais jana aliziagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii na ile ya Fedha kushirikiana Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuchukua
hatua za dharura kupambana nao kwa kuhakikisha vinapatikana vipimo vya
kutosha na dawa.
0 comments:
Chapisha Maoni