Alhamisi, Mei 15, 2014

MSANII WA BONGO FLAVA AFUMWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WA SEKONDARI UFUKWENI

Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Venas John Bebu ‘Bebuz’ amenaswa laivu akivunja amri ya sita (kuzini) na mwanafunzi wa sekondari ufukweni.
Tukio hilo la aibu lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Ufukwe wa Coco, Dar ambapo polisi jamii walimnasa jamaa huyo aliyedaiwa ni swahiba mkubwa wa mwanamuziki, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ ambao hivi karibuni walitoa kibao kipya kijulikanacho kwa jina la Bunyerobunyero.

Mara baada ya kunaswa, Bebuz alianzisha varangati kubwa lakini polisi jamii walimtuliza kwa virungu kisha kumfunga pingu na kumtaka atulize mzuka atoe ushirikiano vinginevyo angeumia.
Ufukwe wa Coco umekuwa ukilalamikiwa kwamba hukutanisha watu wenye malengo mbalimbali lakini wanaokwenda kwa ajili ya kufanya ufuska usiku ni wengi hasa siku za wikiendi ambako kunakuwa na burudani ya disko.
Katika siku za hivi karibu, machangudoa wamekuwa wengi ufukweni hapo na baadhi yao ni vibaka ambao wamekuwa wakitoka nduki na nguo za wanaume huku wakisachi na kuchukua kila kitu.

0 comments:

Chapisha Maoni