Alhamisi, Mei 15, 2014

BAADA YA SAMIR NASRI KUACHWA KATIKA KIKOSI CHA UFARANSA FIFA 2014, AZUNGUMZA YA MOYONI

Kiungo wa Manchester City,Samir Nasri amesema kuwa aliamini kwamba hata chaguliwa na timu ya Taifa ya Ufaransa kwaajili ya kombe la dunia.
Meneja wa Ufaransa,Didier Deschamps aliamua kumwacha Nasri nje ya kikosi kitakachoshiriki michuano inayokuja ya nchini Brazil,licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuwa na msimu wa mafanikio na Manchester City.
Na Nasri anafikiri kuwa kwasasa hana jinsi lakini anatazamia kufahamu mustakabali wake wa soka la kimataifa.
Alipoulizwa alipokeaje taarifa za kutochaguliwa alisema
Nilijiandaa kabisa.Nilifahamu kabla,mara nyingine unakuwa na hisia.
Huku akisisitiza
Unapokuwa unataka kuzungumza na meneja,lakini yeye hataki kuzungumza na wewe,unafahamu kuwa hauendi kwenye kombe la dunia
Nilikuwa nimejiandaa kiakili.Ulikuwa ni mshtuko lakini nilikuwa nimejiandaa kiakili hivyo niko sawa.
Mashabiki wengi wa Manchester City wameshangazwa kuhusu kuachwa kwa Nasri mara baada ya kumaliza msimu vizuri akifunga goli la kwanza Jumapili waliposhinda taji baada ya kuifunga West Ham 2-0.
Nasri akaongeza kuwa
Wakati watu wanazungumzia hilo,inamaanisha kwa baadhi ya pointi kuwa ulifanya kitu kizuri,hivyo ni jambo zuri.
Nini naweza kusema?Naheshimu uchaguzi wake.Hakutaka kuniita mimi,ni jambo zuri kwake.
Niitakia kila la heri timu ya Taifa ya Ufaransa na nahitaji kuchukua muda kadhaa sasa kufikiria kuhusu timu ya Taifa kwasababu inakuwa mara ya pili sasa wanaenda kwenye michuano ya kombe la dunia bila mimi kuwemo.
Deschamps alisema wakati anaelezea kwanini alimwacha Nasri:
Ni muhimili Man City,kitu ambacho sio kesi na Ufaransa na alionyesha wazi kuwa hana furaha iwapo atakaa benchi hivyo naweza kukwambia wewe kuwa inaweza kuleta hisia tofauti ndani ya kikosi.
Lakini nasri alijibu,
Ni kazi ngumu sana kukubali.
Kila kitu ambacho amekuwa akisema.Unaweza ukaenda na kumuuliza mchezaji yeyote kama wanakuwa na furaha kuwepo kwenye benchi.Hakuna hata mmoja anaenda na kukwambia ndio.
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal akadai kuwa,
Kama hiyo ndiyo sababu pekee waliyoipata na kuitumia,ni kazi ngumu sana kukubali.
Nahitaji kufikiria kwa kina,katika kipindi cha likizo kuhusu nini utakuwa mustakabali wangu kwenye timu ya Taifa.Kukosa michuano miwili ya kombela dunia,hakika ni kitu kigumu na kinaumiza kwa mchezaji.

0 comments:

Chapisha Maoni