Jumatano, Mei 28, 2014

MFALME MUSWATI III KUFILISIKA

Taarifa kutoka nchi ya kifalme ya Swaziland zinasema kima cha fedha katika benki kuu ya nchi hiyo kimebaki dollar laki $8 pekee.
Kamati inayohusika na sera za fedha imesema hela hiyo iliyobaki inaweza kununua bidhaa muhimu kutoka nje ya nchi kwa mahitaji ya mda wa miezi minne pekee.
Uchumi wa Swaziland umeathirika pakubwa kutokana na kudorora kwa uchumi wa nchi wanaoitegemea sana jirani zao Afrika kusini ambayo ndio soko kubwa la bidhaa za Swaziland.

Zimebaki dola laki 8 pekee katika benki kuu ya Swaziland.
Hata hivyo Patrick Ndzinisa wa benki ya akiba nchini humo ameiambia BBC kuwa hawana wasiwasi kwani kanuni za kimataifa zanatambua uwezo wa nchi kuagizia bidhaa zake kwa mda wa hadi miezi mitatu.
Mwaka 2011 Swaziland iliiomba Afrika kusini msaada wa dharura baada ya kuishiwa na hela.
Swaziland ilipiga marufuku vyama vya kisiasa nchini humo tangu 1973 na imeshtumiwa kwa rekodi yake mbaya ya uvunjaj wa haki za binadamu. Wakereetwa wa kupigia kampeni mageusi ya
ki-democrasia mara nyingi hukamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi kisha kuzuiliwa magerezani.
Mfalme Mswati na familia yake wameshtumiwa kwa ubadhirifu na ufujaji wa fedha huku wengi wa raia wa Swaziland wakibaki kuwa miongoni mwa maskini zaidi duniani.

0 comments:

Chapisha Maoni