Jumatatu, Mei 12, 2014

LAWAMA ZA WAKAZI WA IRINGA KWA SERIKALI ZITAISHA LINI?

Wakati wakazi wa Kata ya Mkwawa iliyopo Manispaa ya Iringa, wakiomba Serikali kuwapatia vifaa vya usafi, ili kuweza kuondokana na changamoto ya uchafu wa mazingira inayowakabili kwa sasa tayari Manispaa ya Iringa imefanikiwa kununua gari lingine kwa ajili ya kubebea takataka.
Akizungumza kwa niaba ya Wananchi hao, Mwenyekiti wa mtaa wa Makanyagio, Bw.Israel Mbungu, amesema kuwa hali hiyo ya uchafu ni hatari kwa afya za wakazi hao kama hatua stahiki hazitachukuliwa kwa haraka ili kuweza kudhibiti tatizo hilo.
Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Mh.Gervas Ndaki amesema katika kukabiliana na tatizo tayari halmashauri ya Manispaa ya Iringa imefanikiwa kununua gari lingine la kubebea takataka ambalo mpaka sasa lipo bandalini wakifanya utaratibu wa kuondolewa kodi.
Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Iringa Mh.Amani Mwamwindi amesema kuwa, Serikali imejipanga kikamilifu ili kuhakikisha inaongeza vifaa vya kutosha ili kukabiliana na tatizo la takataka ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vizimba vya kuhifadhia takataka kwa maeneo ambayo hayana contena za takataka.
Hata hivyo amewataka wananchi kuwa waangalifu katika uhifadhi wa taka ili kuepuka magonjwa ya milipuko hali itakayo ifanya Manispaa ya Iringa kuwa katika hali ya Usafi.

0 comments:

Chapisha Maoni