Alhamisi, Mei 29, 2014

LAMBORGHINI IMETENGENEZA GARI MAALUM LA POLISI

Kampuni ya magari ya Lamborghini imetengeneza gari hili maalum Huracan LP 610-4 kwa ajili ya polisi wa Italia. Magari haya yatachukua nafasi ya magari ya zamani aina ya Lamborghini Gallardo ambayo tayari yanatumika kupiga doria, limeripoti shirika la habari la Italia, ANSA. Kasi yake ni kilomita 325 kwa saa. Lina kila aina ya teknolojia ya kisasa pamoja na kamera za video kupiga picha wakati ikifukuza wahalifu.

0 comments:

Chapisha Maoni