Ijumaa, Mei 02, 2014

JIHADHARI SANA NA MAPENZI YA MTANDAONI

Polisi nchini Ufilipino, wamesema kuwa wamewakamata washukiwa wa uhalifu katika mitandao ambao ni sehemu ya kikundi cha watu wanaowahadaa watu kwenye mitandao ya kijamii kote duniani.
Washukiwa hao huwashawishi watumiaji wa Internet au walengwa wao katika nchi za kigeni kujipiga picha wakiwa uchi na wakiwa katika vitendo vya mapenzi na kujirekodi kisha kuwatumia.

Wahalifu hao baadaye hudai kiasi Fulani cha pesa kutoka kwa walengwa la sivyo huwatishia kuwa watawatumia jamaa wao picha na video hizo.
Polisi wamefanikiwa kuwakamata washukiwa 58 katika operesheini hiyo iliyohusisha polisi wa kimataifa Interpol.
Lengo la washukiwa hawa ni kutengeza akaunti kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwatafuta wateja wao hasa wazee katika nchi za kigeni
alisema afisa mmoja wa polisi.
Kijana mskochi aliyejiua baada ya kuhadaiwa mtandaoni
Katika akaunti zao hizo wao hujidai kuwa ni wasichana wenye asili ya Asia wanaotafuta wapenzi katika nchi za kigeni.
Baada ya kujuana vyema na watumiaji wa mitandao wasiojua kuwa wanahadaiwa, wao huwakaribisha kuwa marafiki zao kwenye mitandao , kuwasiliana nao kwa njia ya video kwenye mitandao hiyo hiyo na kisha kufanya nao vitendo vya mapenzi kupitia kwa kompiuta huku wakirekodi kila kinachofanyika
Kanda hizo sasa hutumiwa kama njia ya kupata pesa kutoka kwa waathiriwa kwa kutumia vitisho kuwa watasambaza kanda hizo kwa watu wa karibu wa waathiriwa la sivyo walipwe kati ya dola 500 na 2,000. Pia hutishia kusambaza kanda hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Afisa mkuu wa Interpol amesema kuwa uhalifu huo umeenea sana kwenye mitandao. Uhalifu wa aina hii hauna mipaka umeenea kote , sio Ufilipino peke yake.
Kijana mmoja kutoka Scotland, alijiua baada ya kujikuta katika hali ya kuhadaiwa kwenye mitandao kwa njia hii.

0 comments:

Chapisha Maoni