Jumapili, Mei 18, 2014

FUNDI CHEREHANI AFANYA MAMBO KWA DAVINA WA BONGO MOVIE

Halima Yahya ‘Davina’ amechefuliwa vibaya na fundi wa nguo kwa kumcheleweshea nguo ya sare na kumfanya ashindwe kuivaa kwenye shughuli ya msanii mwenzake, Vanitha Omari.
Akipiga stori na mwandishi wetu katika shughuli hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mawela Sinza, jijini Dar, Davina alisema amelazimika kuvaa nguo ya tofauti kutokana na fundi kushindwa kumshonea nguo yake kama alivyotaka.
Lakini nashukuru Mungu sana kuona nimependeza na kila mtu anataka kupiga picha na mimi pamoja na fundi kunifanyia mtima nyongo, amenitibua kweli
alisema Davina aliyetinga ukumbini na gauni nyeusi.
WAGENI mbalimbali waalikwa wamejikuta wakiangua vilio upya baada ya kumkumbuka aliyekuwa mwigizaji, Zuhura Maftah ‘Melisa’.
Tukio lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mawela, Sinza jijini Dar wakati dada wa marehemu (Haris) alipokwenda kutoa zawadi kwa niaba ya marehemu kwenye kitchen party ya mwigizaji Vanitha Omari.
Mungu alimpenda zaidi mdogo wangu kabla hajafanikisha zoezi hili ila nimeamua nimtolee zawadi rafiki yake kwani alipanga kumchangia Vanitha
 alisema Haris na kusababisha biharusi mtarajiwa aangue kilio pamoja na baadhi ya waalikwa.
Melisa alifariki dunia mwaka jana baada ya kuugua na kulazwa kwa muda mfupi.

0 comments:

Chapisha Maoni